Habarini za leo wapenzi wasomaji wa gazeti hili la kwanza kwa ukubwa nchini Tanzania,ni matumaini yangu kuwa nyote mmevuka wiki salama baada ya mshikemshike wa siku za Wanasimba(Simba Day) na Wananchi(Yanga Day);zilizolindima kwa siku tofauti tofauti za tarehe 03 Agosti na 04 Agosti,2024.Katika makala haya ya leo nitajikita zaidi kuangalia jinsi matamasha hayo yalivyoandaliwa na ufanisi wake ulikuwa kwa ukubwa gani;nani alifanya vizuri zaidi ya mwenziye na kwa vigezo gani kama itakavyoainishwa hapa chini.
MANDHARI:-Tukianza na Simba Sports Club kwa upande wa Mandhari walifunika sana kwa kupamba majukwaa yao kwa rangi zao pendwa za Nyekundu na Nyeupe kiasi cha kuufanya uwanja kuonekana kimahaba zaidi;kwa kuwa rangi zao nyekundu na nyeupe zilikuwa zinawaka kwelikweli,zilizidi kuyapamba mandhari hayo na hivyo kuwavutia zaidi watazamaji wao.
Kwa upande wa Watani wao wa jadi yaani Young Africans Sport Club almaarufu Yanga au Wananchi,majukwaa yao yalipambwa kwa rangi zao za biashara yaani Kijani na Njano;tofauti na Simba ambao mpangilio wa majukwaa ulikuwa mzuri sana,Yanga majukwaa yao hayakuwa na muonekano angavu au hayakuwa ng’aring’ari kama wenzao wa Simba.
AMSHA-AMSHA NA USHEREHESHAJI:-Wakati Simba Day ilishereheshwa zaidi na Afisa habari na msemaji wa timu hiyo kijana mtukutu mwenye mbwembwe bin machezo mengi Ahmeid Ally;aliweza kufanya amsha-amsha za kutosha zilizoambatana na vijembe kwa watani wake kwa maneno kama; ‘Ninajua sisi Wanasimba ni watu bora tusiokunywa supu ya kibudu!’
Wakati Ubaya-Ubwela ulisimamiwa na jeshi la mtu mmoja,kwa upande wa Wananchi wao walikuwa hawapoi wala hawaboi kwa kushusha washereheshaji wa aina mbalimbali kutegemeana na matukio.Walikuwepo akina Dakota De Lavida kama muamshaji mkuu(Hyper),baadaye wakaja watangazaji wa bei kali akina Maulid Kitenge a.k.a mzee wa Earphone akiwa sambamba na pacha wake Zembwela chini ya uangalizi mkuu wa Al-Bugati Haji Sunday Manara;ilikuwa balaa.
WASANII WAALIKWA NA KAZI ZAO:-Wakati Simba walikuwa wamewaalika wasanii wa muziki wa aina mbalimbali,msanii kinara kwa upande wa Simba siku hiyo ya Agosti-3 alikuwa mfalme wa Bongo Fleva Ally Kiba ambaye alifanya shoo ya kibabe sana akiwa na wachezaji waliokuwa wamependeza sanaa kwa nguo za bei kali zenye rangi ya biashara ya Simba.Siku hiyo Mfalme Kibba alikuwa ameongozana na madansa warembo waliokuwa wameoga wakataka haswaa lakini zaidi sana walicheza kwa ustadi wa hali ya juu,kwa mara nyingine King Kibba alidhihirisha ni kwa nini miaka hiyo ya nyuma aliweza kuimba na akina R-Kelly wa huko Marekani!
Yanga nao siku hiyo walishusha wasanii wa Muziki wa aina mbalimbali ukianzia Bongo-fleva,Singeli hadi muziki wa Dansi ambapo mkali wa masauti kama vile ambavyo yeye mwenyewe hupenda kujiita;huyo si mwingine bali ni Christian Bella Mwingira alikuwepo kufanya balaa.Zaidi sana orodha hiyo ndefu ya wasanii waliotumbuiza siku ya Wananchi ilihitimishwa na Tembo aliyezaliwa Usafini na kutorokea Konde Gang ambaye alibebeshwa msalaba mzito wa kuwatungia Wananchi wimbo utakaoweza kukata ngebe za Watani zao.Tembo huyo hakufanya ajizi maana huwa hana shoo ndogo,aliwapakulia hiti song’ iitwayo “Yanga Bingwa” ambayo inazidi kusumbua vichwa vya Watani hadi kesho.
Licha ya tembo huyo kuachilia wimbo mzuri ambao unapendwa sana kuliko nyimbo zote zilizowahi kutokea lakini kwa upande wa shoo ya jukwaani haikuwa nzuri sana; kwani Yeye pamoja na madansa wake walivaa kawaida sana lakini hata mpangilio wa nyimbo wakati wa kutumbuiza jukwaani haukuwa mzuri-Tembo aliboa.
MPANGILIO WA MATUKIO NA MUDA:-Katika mpangilio wa matukio na muda,Wanasimbaaa walifanikiwa saanaa kwani matukio yote yalipangwa kwa mtiririko mzuri sana;pongezi nyingi ziende kwa mratibu wa tukio hilo(Floor manager),anastahili maua yake.Kwa umakini huo wa Wanasimbaa ulisababisha hata mchezo wao na wageni wao timu ya APR- kutoka Rwanda ulianza saa 1:30 za usiku kama ilivyokuwa imepangwa.
Yanga siku hiyo ni kama vile matukio yao hayakuwa yameandaliwa mapema kwani mara kadhaa tuliaona wakibadili utaratibu au kunong’onezana mara kwa mara ili kuweka mambo sawa;hali hiyo ilipelekea hata mchezo wao na Wageni wao Red Arrows kutoka Zambia kuanza muda wa watoto kwenda kulala.
UBORA WA WACHEZAJI NA BENCHI LA UFUNDI:-Wakati Simba wamekibomoa kikosi chao kwa zaidi ya asilimia 85,walikuja na wachezaji wengi wapya wakiwamo akina Joshua Mutale chini ya benchi jipya kabisa la ufundi linaloongozwa na Kocha Fadlu Davids; mzaliwa wa Afrika Kusini aliyewahi kusakata kabumbu katika baadhi ya vilabu huko kwao.Mpaka anatua mtaa wa Msimbazi alikuwa anatokea nchini Morroco ambako alikuwa kocha msaidizi wa Mabingwa wa soka nchini humo yaani Raja-Cassablanca.
Kutokana na ubora wa timu aliyokuwa akiitumikia huko nchini Morroco,wachambuzi wa Soka kutoka nchi mbalimbali za Afrika wanaamini kuwa;Kocha Fadlu anaweza kuwa mpinzani bora kabisa kwa kocha Gamondi.
Yanga wao wana kikosi kinachotisha kama ukoma wala haupati shida kukielezea,majina ya wachezaji wake yanavuma kwenye mitaa kuanzia kwa watoto,akina mama hadi wazee.Ubora wa kikosi hicho meyafanya mauzo ya jezi zao kuvunja rekodi ya kununuliwa,mfano mzuri ni fulu hausi iliyoshuhudiwa pale uwanja wa Mkapa ambapo Wananchi waliujaza uwanja huku jezi mpya zikiwa zimetapakaa kila kona.Iwe jua au iwe mvua,Wananchi ndiyo timu pekee yenye kikosi kinachotisha zaidi katika ukanda wote wa nchi za CECAFA na SADCC.
UHUSIANO WA WACHEZAJI NA VIONGOZI:-Katika hili,Yanga wamefanikiwa kwa karibu asilimia 85,za ndani kabisaa zinasema;sababu mojawapo iliyomfanya mwamba wa Ouagadougou Aziz-Ki kusalia Jangwani ni uhusiano mzuri uliopo kati yake na benchi lote la ufundi bila kusahau uongozi wa juu wa timu hiyo chini ya Rais kijana sana Mhandisi Hersi Sayyid.
Hilo la Wananchi kuishi kama familia ya baba na mama mmoja,linathibitishwa na kitendo cha hivi karibuni ambapo kocha Gamondi anaonekana akiigiza kwenda kuangalia Refarii Msaidizi wa Video(VAR) baada ya Aucho kumchezea rafu mwenzake wakati wa mazoezi huko Avic-T0wn;kituko hicho kinamfanya Ally Kamwe kumshabikia Gamondi aende kuangalia VAR-hiyo ya makaratasi yaani ni fulu vicheko.
Kali kuliko zote ni pale wachezaji wa Yanga akina Aucho na YaoYao wakiwa wamemkandamizia chini Rais wa Yanga Mhandisi Hersi Sayyid huku wakihanikiza kuletewa maji wamuogeshe bosi wao katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa-hii ni nadra sana kuikuta kwa vibosile wengine.Mbiringembiringe kama hizo na nyingine nyingi zinawafanya Wananchi kila siku kuiteka mitandao ya kijamii na kuwa maarufu zaidi
Kwa Wanasimbaa hali kama hiyo siyo rahisi sana kuiona ingawa na wao wana mtindo wao wa maisha unaowatofautisha na watani wao.
Nihitimishe kwa kusema kwamba,watu hujifunza kutokana na makosa aidha ya kwao wenyewe au ya watu wengine;Simba Sports Club wanapaswa kujitathmini na kuona wapi wanapwaya ili waweze kufanya marekebisho ili warudie zama za ubora wao enzi hizo wakiwa chini ya mwanamke wa nguvu(Iron Lady) Barbara Gonzalez-ilikuwa nzuri hiyoo!
Ninawatakia kila lakheri katika kuhakikisha kuwa kazi zinaendelea,tupo pamoja na hakikisha mtu wangu wa nguvu haukosi nakala ya Gazeti hili kila wiki-Mungu ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika na Dunia nzima!
Mwandishi wa makala haya ni Mwinjilisti(Evangelist),Mwandishi wa Makala na Vitabu(Author and Columnist),Mtoa Hamasa(Motivational speaker) na Meneja wa biashara(Business Manager).Kwa sasa ni Meneja wa LUMASAMA MICROFINANCE LIMITED huko Runzewe-Geita.
Maoni au ushauri nipigie:- +255 689 881790(WhatsApp) au +255 763 018999 au mcmashamba8@gmail.com
KWA YANGA HII,VIONGOZI HAWA NA WACHEZAJI HAWA;SIMBA WATASUBIRI SANA!
Na:Prince Ngeni Mashamba.
Habarini za leo wapenzi wasomaji wa gazeti hili la kwanza kwa ukubwa nchini Tanzania,ni matumaini yangu kuwa nyote mmevuka wiki salama baada ya mshikemshike wa siku za Wanasimba(Simba Day) na Wananchi(Yanga Day);zilizolindima kwa siku tofauti tofauti za tarehe 03 Agosti na 04 Agosti,2024.Katika makala haya ya leo nitajikita zaidi kuangalia jinsi matamasha hayo yalivyoandaliwa na ufanisi wake ulikuwa kwa ukubwa gani;nani alifanya vizuri zaidi ya mwenziye na kwa vigezo gani kama itakavyoainishwa hapa chini.
MANDHARI:-Tukianza na Simba Sports Club kwa upande wa Mandhari walifunika sana kwa kupamba majukwaa yao kwa rangi zao pendwa za Nyekundu na Nyeupe kiasi cha kuufanya uwanja kuonekana kimahaba zaidi;kwa kuwa rangi zilikuwa ni nyekundu na nyeupe hasa zilizokuwa zinayachoma macho ya watazamaji.