HONGERENI SANA KWA KUTULETEA VICHWA HIVI MTAANI!
Na Prince Ngeni Mashamba.
Habarini za wiki hii wapenzi wa gazeti pendwa la Pambazuko popote mlipo katika nchi yetu tajiri yenye kila aina ya baraka na utajiri tuliopewa bure bileshi na Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema;kama mimi nilivyo mzima wa afya,ni matumaini yangu kuwa hata ninyi kwa neema zinazodumu milele za Jalali mu-wazima wa afya kabisa.
Stay in touch to get latest news everyday.
Nianze kwa kuwaomba radhi wapenzi wasomaji wa makala zangu mlioko ndani na nje ya nchi kwa kutokuandika makala mpya kwa muda mrefu, kwa sababu za kiufundi na kiuchumi zaidi katika magazeti yaliyo mengi hapa nchini kwetu-mengi ni “fulu” ubabaishaji.
Kama mada yetu ya wiki hii ilivyo hapo juu na hasa ikizingatiwa kuwa,habari ya mjini mwaka huu kama wasemavyo watoto wa mjini ni Uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani kwa Tanzania bara lakini kwa upande wa pili wa nchi yetu;ni uchaguzi wa Wawakilishi katika majimbo ya Zanzibar na Wabunge wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Leo nitaanza kwa kuyamulika yaliyotokea kwenye kura za maoni zilizopigwa na “wajumbe” wa chama tawala (CCM) katika mchakato mzima wa kuwapata wagombea wa udiwani na Ubunge katika Kata na majimbo mbalimbali kwa upande wa Tanzania bara.
Welcome again Subscribe to get latest news.
Kufuatia kura hizo za maoni kupigwa siku ya tarehe --------- na matokeo au majina ya waliopitishwa kugombea nafasi hizo kutolewa usiku wa kuamkia siku ya ------;baada ya kamati kuu ya (CCM) kufanya mapitio ya mwisho na majina kurudishwa rasmi ya wagombea watakaoipeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambao huenda usiwe na mvuto wa kuitwa Uchaguzi mkuu bali Uchafuzi mkuu; kutokana na chama kikuu cha upinzani kufungiwa kufanya shughuli zake za kisiasa kama ilivyo ada na kinara wa chama hicho Wakili Tundu Antipas Mghwayi Lissu akiendelea kutaabika nyuma ya nondo za gereza, kwa kushitakiwa kwa kesi ya Uhaini huku watuhumiwa wa mauaji ya Hayati John Joseph Pombe Magufuli wakiendelea kula biriani na urojo kwenye viunga mbalimbali vya Tanzania bara na Visiwani.
Advertise Your Business Here.
Ingawa siyo shabiki wala muumini wa (CCM) tena tangu hayati (JPM) apumzike kwa lazima,leo kwa shingo upande nimeamua kukipongeza chama tawala a.k.a Wahuni kama anavyotuhubiria na kutupa darsa Balozi Humphrey Herson Polepole;mimi ni nani hata nikatae kuwaita wahuni ikiwa mwenzi wao anayewafahamu nje ndani huwaita hivyo na wao kukaa kimya kabisa bila kujitetea kwa namna yoyote ile-kukaa kimya ni ishara ya kukubaliana na kile kisemwacho na Komredi au Kada mkaidi wa (CCM).
Get latest news everyday.
Kilichonifanya niwape kongole wazee hawa wa kijani na njano a.k.a Mama anaupiga mwingi;ni kitendo chao cha kuyakata kwa ukaidi,uhuni na ubabe unaochagizwa na ulevi wa madaraka baadhi ya majina ya wabunge maarufu na mahiri waliokuwa wamepewa kura za ndiyo na wajumbe katika majimbo yao.
Wabunge hao ni Dada yetu Ummy Mwalimu a.k.a Oddo wa jimbo la Tanga mjini,Professa Kishimba kama alivyokuwa akiitwa na hayati Spika Ndugai wa jimbo la Kahama,mdogo wangu Dr. Hamis Kigwangalla(mimi kidato cha 6 yeye akiwa kidato cha 5 wakati tukiwa ShyBush);wa jimbo la Nzega vijijini,Tata mura wetu Kembaki wa jimbo la Tarime mjini,Mangi Professa Ndakidemi wa jimbo la Moshi vijijini na wengine wengi lakini hawa niliowataja ndiyo nina jambo nao kama nitakavyodadavua hapo chini.
Subscribe to our mail list to get news.
Professa Jumanne Kishimba a.k.a Ngosha ze Don; kurudi kwake mtaani kwangu ni furaha kubwa sana na kongole kwa (CCM-wahuni kwa mujibu wa Polepole na siyo mimi akuu!). Kurudi mtaani kwa Professa Kishimba,ni ukombozi mkubwa kwa sekta ya biashara na uchumi hasa ikizingatiwa kuwa,mheshimiwa huyu ana weledi mkubwa katika masuala ya kibiashara na uchumi hali iliyopelekea miaka ya tisini wakati nikiwa “dogoras” sana jina la Kishimba kuwa linatumiwa kwa watu wenye pesa chafu kama sasa hivi ilivyo kwa majina kama Dangote,Bakhressa na Mo-Dewji.
Ninawapongeza (CCM) kwa sababu kwa kufanya hivyo,ninaiona kabisa ile Kishimba International Traders ikirejea upya na kuanza kuleta ushindani wa kibiashara kwa matajiri wenziye akina Mo-Dewji,Dangote na Bakhressa.
Lakini pia ninaona kabisa vile viwanda vya kuchakata pamba(Ginneries) vilivyokuwa vimeajiri maelfu ya Watanzania akianza kuvifufua na kuongeza pato la taifa na ajira kwa wahitimu wengi wa chuo wanaohangaika kutwa kucha mtaani wakifukuzia ajira.
Mangi Professa Ndakidemi huyu kurejea kwake mtaani kwetu sisi tuliokuwa wanafunzi wake na aliotusimamia wakati tunasoma shahada zetu za pili(Masters);ni fulu shangwe kwa sababu tunaamini kuwa,badala ya akili hii kubwa kuendelea kubaki mjengoni na kupiga makofi na kujibu “ndiyoo!” ilikuwa ni matumizi mabaya sana ya akili hii kubwa-haipaswi kuigwa na jamii!
Kama Waswahili wasemavyo, “tabu huleta maarifa!” Baada ya kukaa mtaani lazima atajiongeza tu kwa namna yoyote ile ili mkono uweze kwenda kinywani aidha kwa kurudi kufundisha au kufungua chuo au kuwa Mhadhiri mshauri-karibu sana mtaani Mangi Ndakidemi,aikambee.
Mdogo wangu Dr. Hamisi Kigwangalla karibu sana kijiweni ili tuanze kuumiza kichwa pamoja katika harakati takatifu za kuifukuzia shekeli na siyo zile za kusaini tu hata kama haukuwemo mjengoni;na mbaya zaidi ninafahamu utamisi ule msosi na kifungua kinywa cha mjengoni-huwa kimekamilika idara zotee!
Mdogo wangu ninafurahi kukuona mtaani kwa sababu ninaamini kabisa huu ndiyo ule wakati wa kampuni yetu ya (MSK-company) ikirudi sokoni kwa kishindo mithili ya Simba aliyeuliwa mtoto wake au nyoka koboko aliyekanyagwa ghafla mkiani.
Zaidi sana tutakuwa na muda mwingi wa kuongea na wewe na kupata madini ya kitabibu maana wewe ni Daktari kabisa wa kusomea na siyo kama yule daktari wa kimiujiza aliyezaliwa darasa la saba lakini alivyokua ghafla akawa daktari-Wasukuma wana mshangao usemao “hilu maza!”
Mura wetu Kembaki kwa kweri mura riujio rako rimetufurahisha sana mura maana sasa tunaamini kabisa ile miradi yako uliyokuwa umeitelekeza huko na Tarime na visiwani inakwenda kufufuka upya.Hii itatusaidia sisi wapambe wako tuliokuwa tumepauka kwa kusota mtaani kuanza kuvimba tena mtaani mura wetu-karibu sana mura.
CCM-ONGEZENI TENA;nimalizie pongezi zangu kwa kukiomba chama changu pendwa kiendelee kutuletea vichwa adimu ambavyo vimeamua “makusudically” kuacha kutumia karama zao adimu walizojaliwa na Manani kutengeneza utajiri na ajira mtaani lakini vimeamua kwenda mjengoni kupiga makofi na kusema “ndiyoo!” kisha vinasaini na hela zinaingia mfukoni.
Chama changu pendwa ninaomba wakati mwingine ikikupendeza utuletee mtaani hivi vichwa vifuatavyo:- Eric James Shigongo(Magazeti yote yamekufa),Kaka yetu Abood Bus Service(Mabasi yamepungua),Professa Palamagamba John Mwaluko Kabudi(tuna uhaba mkubwa wa maprofessa vyuoni),Professa Kitilla Mkumbo(Hamna watafiti wa kibiashara na uchumi).
Asanteni sana wapendwa kwa kunisoma,ninawatakia maandalizi mema ya Uchaguzi mkuu kwa wale mtakaotiki na wale wa No Reforms,No Election-endeleeni kubarikiwa na Mwenyezi Mungu!
Mwandishi wa Makala haya ni kiongozi mwandamizi wa Kumekucha Online Newspaper na Mwalimu kiongozi wa The King Solomon Ministry.
Maoni au ushauri nicheki kwa njia zifuatazo:- +255 689 881790(WhatsApp) au mcmashamba8@gmail.com
Advertise Your Business Here.
Sound Power Media Productions Tanzania is a media company based in Video Production, Entertainment, Information Technology and Sales of Electronics Devices based in Arusha, Moshi and Dar es salaam.
Our Services:
Video Shooting and Editing
Color Grading and Visual Effects
Advertising and Promotion
Content Creating and Marketing
Website Design and Hosting
Mobile App Development
Social Media Marketing
Music Distribution and Promotion
Rental Services for Events
Music System, Stage and Lights
Call: 0681 845691 - 0748 200938 - 0777 017979
Email: soundpowermediaproduction@gmail.com
Subscribe to Get your latest news everyday