China inaweza kukupa utajiri sana, lakini pia unaweza kupoteza mtaji wako wote.
.
Sasa kabla hujaenda china, hakikisha unayajua haya mapema ili safari yako iwe ya mafanikio makubwa.
.
1. Pata passport yako Mapema, Ni vizuri pia kama Mfanyabiasha mwenye malengo makubwa kuwa na passport.
2. Fatilia Visa yako. Ubalozi wa china uko Masaki. Pata visa yako mapema ili ukate tiketi mapema upate kwa bei nzuri.
3. Pata tiketi yako mapema ya ndege. Mashirika ya ndege ni mengi na kila shirika lina uzuri wake uharaka, mizigo, chakula na huduma. Nauli ya kwenda China na kurudi ni kati Tsh 3M ( bei hubadilika kulingana na season na muda uliokata na shirika)
4. Usiende china hujui utanunua nini, Usiende china kwa lengo la kuagizisha bidhaa kwa oda hasa kama ni mara ya kwanza. Kama una mtaji mkubwa Fahamu ni mji gani bidhaa zako utapata na utafikaje kwenye huo mji kutoka Ghuanzou
5. Download app ya Wechat, Hii ni kama whatsapp kwa china, Itakusaidia kukusanya mawasiliano ya supplies lakini pia kuwasiliana na translation
6. Pata laini ya China ukifika. Itakusaidia kwenye mambo mengi.
7. Kabla hujaanza safari ni muhimu kutambua ni nani ambaye atakupokea, na utafikia hoteli gani.
8. Download VPN kabla ya kwenda China kwani huko hutoweza kutumia Google, Whatsapp, instagram, tiktok nk bila VPN hata ukiwa kwenye Wi-Fi ( naweza kukupatia pia laini za china au Dubai kabla hujaenda ili ukifika uwasiliane na wenyeji wako na utumie mitandao yote bila VPN usije ishia Airports, Tunazo dukani)
9. Download app ya DiDi ( ndio Uber /bolt za china) itaokoa gharama zako kuliko kutumia Tax za kawaida
10. Tafuta mtu akufundishe kutumia metro🚇( ni Tren za haraka za ardhini kama daladala) ni Rahisi na nafuu mno
11. Kwa ushauri, kama una mtaji wa chini ya 15M na hutaki kuupoteza usiende china kwanza, kwa competition ya sasa ni ngumu bidhaa za 10M kukupa 20M ambayo itarudisha gharama zako, mtaji na faida. Ila China ni sehemu nzuri kwenda kujifunza Biashara hivyo kama lengo ni kujifunza na kupata suppliers kwa biashara yako nenda tu hata na mtaji mdogo.
12. Kwa mara ya kwanza, usiweke kukaa chini ya week moja labda kama una mwenyeji. China masoko yako mbali na huchelewa kufunguliwa, utahitaji kutumia muda mwingi kupata machimbo.
13. Ukifika kusanya business card za kutosha za suppliers. Zitakusaidia ukirudi
14. Beba kiasi cha pesa ya Kichina (RMB) kabla ya kwenda. Zitakusaidia kwenye mengi kuanzia usafiri ukifika ( change Bank na utapata rate nzuri kuliko ukiwa CHINA)
15. Njia za malipo ukiwa china ni cash na mobile payment kama Alipay & Wechat pay zaidi ( hakikisha unakua na Alipay)
16. Beba dawa zako kama unajijua una ka_ugonjwa Kako au unashikwa mafua kirahisi, kichwa nk.
17. Ukiwa china jichanganye na wenzako hasa wenyeji wa china, Hii itakusaidia kujua fursa zaidi na machimbo.
18. Kunywa maji ya chupa ya dukani na usipendelee kunywa maji ya Bomba.
19. Utapata wapi viwanda? Bidhaa unayohitaji iko wapi?
Jambo gani unatamani kujua zaidi kabla ya kwenda China?.